June 29, 2018


Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) limetangaza kuwa, katika michuano ya Kagame inayotarajiwa kuanza leo Ijumaa, itachezeshwa na waamuzi 18 kutoka mataifa mbalimbali.

Michuano hiyo ambayo imepangwa kufanyika kwenye viwanja vya Taifa na Azam Complex jijini Dar es Salaam, itahitimishwa Julai 13, mwaka huu.

 Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye alisema mbali na kuwatangaza waamuzi hao, lakini haitavumilia kuona timu shiriki zikileta wachezaji vijana chini ya miaka 20.

“Waamuzi tayari tumewaandaa ambapo watakuwa 18 kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa mashindano. Kikubwa tunataka kuwa na mashindano yenye ushindani.

“Nizikumbushe timu shiriki tu kuwa, zinapaswa kuja na vikosi vyao kamili na hatutavumilia endapo ikitokea timu imeleta kikosi cha vijana chini ya miaka 20,” alisema Musonye.

Michuano hiyo inaanza rasmi kwa mechi tatu kupigwa ambapo saa 8 mchana JKU ya Zanzibari itaanza kibarua chake dhidi ya Vipers SC kutoka Uganda.

Baadaye saa 10 mechi ya rasmi ya ufunguzi itakuwa baina ya mabingwa watetezi, Azam FC dhidi ya Kator FC kutoka Sudan Kusini. Baada ya mechi hiyo majira ya saa 1 jioni, Singida United itacheza na APR ya Rwanda.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic