June 29, 2018





NA SALEH ALLY
NIMEPATA taarifa kwamba uongozi wa Simba ulifikia uamuzi wa “ukweliukweli” kwamba safari hii hawataki mchezo na wameamua kuachana na beki Juuko Murshid.

Simba wameamua kuachana na beki huyo wa kati wakiamini amekuwa si msaada katika mambo mengi sana.

Suala hilo wamelijua kwa muda mwingi lakini waliendelea kubaki naye huku ikionekana kwamba hawakuwa na namna ya kuweza kumuacha Juuko ambaye naye alilijua hilo.

Wakati mwingine kama unataka kujua mambo mengi, vizuri pia kujifunza kupitia viongozi walio katika mchezo wa soka.

 Kawaida viongozi hao wanaweza kuonekana ni kama wanaokosea kila siku. Lakini kama utafuatilia unaweza kugundua ni watu wanaonewa kila mara na wao wamekubali kuwa waoga ndiyo maana wanaweza kuendelea kuharibu mambo kila mara.

Nitakuambia kwa nini. Ndani ya klabu hizi kubwa, wako wachezaji wengi wanaokosea sana. Lakini wanaweza kuficha makosa yao katika hadhira kwa kuonyesha wana mapenzi au wanazitumikia sana timu zao mbele ya mashabiki.

Lakini ndani yake wakavunja utaratibu wa viongozi. Wakachelewa, wakaondoka bila ya kuomba ruhusa au kutoonyesha kwamba wanajali maagizo fulani ya uongozi. Wanafanya hivyo wakijua kwamba watetezi wao ni mashabiki na wanachama.

Hivyo, kwa kuwa wanajua wana watetezi. Basi mbele yao ni kuonyesha wao ni watu wanaojali sana, pia wanapambana kwa ajili ya klabu yao.

Hii maana yake ni hivi, uongozi utakapoonyesha au kutangaza unataka kuwaacha. Basi inakuwa ni ugomvi mkubwa baina yao na wanachama au mashabiki.

Nakuambia hivi, viongozi wa hizi klabu wanakutana na mambo mengi baadhi wanahitaji kuonewa huruma. Lakini ninashangazwa nao kushindwa kuwa imara na kusimamia kile kilicho sahihi bila ya kujali wanachama na mashabiki watakasirika, eti kwa kuwa fulani ameadhibiwa.

Angalia Juuko raia wa Uganda, mara kadhaa ameshindwa kurejea kwa wakati kambini. Amechelewa kwenye sehemu alizotakiwa kutekeleza jambo na kadhalika.

Amekuwa maudhi kwa viongozi na wakati mwingine mfano mbaya kwa wachezaji. Huenda ni kawaida yake lakini hakupaswa kufanya hivyo.

Mtu ambaye akiamua anacheza kweli, anakuwa msaada mkubwa. Halafu anaweza kuamua kufanya mambo yake anavyotaka yeye.

Hivi karibuni, viongozi wa Simba walishindwa kupata mawasiliano yake. Lakini wameishi kama mzazi na kukaa kimya wakiendelea kumtafuta bila ya mafanikio. Hali kama hii imetokea mara kadhaa lakini bado ikawa siri yao.

Ninajua, mara kadhaa walitaka kumuacha Juuko wakionekana kuwa wamechoshwa na vituko. Lakini hofu ya kugombana au kuwaudhi wanachama na hasa kama atasajiliwa na Yanga ndiyo ilikuwa hofu yao kuu.

Mwisho wakaendelea kubaki nao akiwatafuna ndani kwa ndani kama ambavyo Donald Ngoma alikuwa kwa Yanga akiendelea kupokea malipo, kwa kuwa ni mgonjwa na bado akiwa mngonjwa wakamsajili na kumpa mawilioni.

Kisa cha Yanga kufanya hivyo kwa Ngoma ilikuwa ni hofu ya kuwadhi wanachama. Lakini viongozi hawakuwa wakiangalia suala la anaisaidiaje timu. Badala yake “wanachama watatuelewaje” inabaki kuwa ishu ya msingi!

Kuwa kiongozi bora ni kufanya mambo kwa usahihi. Kawaida usahihi ni kufanya mambo ambayo yanakwenda nje ya mazoea au yanakuwa na maudhi kwa kuwa hayaendani na mazoea.

Kubadili mambo kama ni kiongozi unatakiwa kuwa imara kweli kwa kusimamia yale unayoyaamini. Wakati mwingine unaweza kupingwa na kila mtu lakini ukasimamia na kukitekeleza ulichoamini ni sawa.

Kama utafanya kwa ufasaha bila ya hofu ya kupingwa. Inakuwa kuna wepesi katika kufanikiwa. Lazima viongozi mbadilike na kuwa imara kwa ajili ya mafanikio ya sasa na baadaye badala ya kuangalia zaidi kukwepa kuwaudhi wanachama. Mabadiliko, kawaida ndani yake yamechanganya maumivu.

2 COMMENTS:

  1. Unafiki mtupu nyinyi waandishi ndio mtakaokuwa wa kwanza kuja kuwachamba sumba kwa kumuacha Juuko. Binafsi nilidhani Juuko na Pascal wawa wangetengeneza ukuta wa zege pale Simba. Kama simba wanaamua kuachana na juuko waachane nae tu lakini sio kitu cha kupongeza. Na ni ujinga mtupu kumfananisha Juuko na Simba na Ngoma na Yanga? Juuko kakulia pale simba kaja akiwa kinda na ni miongoni mwa wachezaji wachache waliodumu pale Simba kwa sasa.

    ReplyDelete
  2. waandishi wa michezo ni watu wa kukurupuka simba hawakumtendea haki JUUko walikuwa wanamwacha benchi kwa wachezaji wasio na kiwango wakati huyo mchezaji ana namba timu ya taifa ya Uganda ambayo ilikuwa inafanya vizuri katika mchezo wa simba na lipuli beki aliyepigwa chenga na Salamba hadi akafunga yule beki aliachwa badala yake JUUKo akatolewa unafiki huo ndio uliomfanya awazimie viongozi simu kwani angeendelea kubaki simba angepoteza namba timu ya taifa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic