June 29, 2018


Kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere, 26, anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake katika klabu ya Uturuki ya Fenerbahce siku ya Jumatatu. (Sabah - via Talksport)

Chelsea inakaribia kuipiku Real Madrid katika kumsajili kipa wa Roma Alisson katika mkataba ambao unaomthamini mchezaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 25 kuwa na thamani ya £62m. (Marca - via Metro)

Arsenal inatarajiwa kukamilisha uhamisho wa beki wa Borussia Dortmund Sokratis Papastathopoulos, 30, wiki ijayo. (Star)

Na makubaliano ya dau la £26m ya kumnunua kiungo wa kati wa Sampdoria na Uruguay Lucas Torreira, 22, yanakaribia kukamilika.(Telegraph)

Kiungo wa kati wa Chelsea Jeremie Boga, 21, ameanza mazungumzo ya kuhamia katika klabu ya Itali ya Sassuolo. (Mail)

Ajenti wa beki wa Juventus Daniele Rugani amesema kuwa uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kuelekea Chelsea unatagemea iwapo Maurizio Sarri atakuwa mkufunzi katika klabu hiyo ya Stamford Bridge. (Sport Italia - via Sun)

Kiungo wa kati wa Real Madrid Marco Asensio 22, anapanga kuhamia Liverpool ambapo huenda uhamisho huo ukamfanya kuwa mchezaji mwenye pochi kubwa katika historia ya klabu hiyo. (Marca - via Express)

Mchezaji anayenyatiwa na klabu ya Manchester United Milan Skriniar amesema kuwa anafurahi kuwa katika klabu ya Inter Milan na anasema kwamba anataka kusalia katika klabu hiyo.

Beki huyo wa kati amesema kuwa Red Devils ina hamu ya kumsajili. (Radio Expres - via Star)

Kutoka BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic