June 29, 2018






Kocha Dylan Kerr ametoa onyo, ameweka msisitizo kuhusiana na suala la kiungo Francis Kahata.

Kerr ambaye sasa ni kocha wa mabingwa wa Kenya, Gor Mahia amesema Kahata bado ana mkataba na klabu yake na Simba wanapaswa kuheshimu hilo.

"Lazima waonyeshe nidhamu ya mkataba, Kahata ana mkataba na Gor Mahia, wasifanye mambo kienyeji.

"Kuna mambo yamekuwa yakiendelea. Hili si jambo sahihi na lazima vitu vifuate weledi," alisema.

Kumekuwa na taarifa kwamba Simba inaendelea kumnyatia Kahata ambaye ni kiungo mchezeshaji tegemeo wa klabu hiyo kongwe na maarufu zaidi nchini Kenya.

KERR AKIWA NA SALEHJEMBE

Tayari Simba imefanikiwa kumsajili Meddy Kagere ambaye ni mshambulizi tegemeo wa Gor Mahia, jambo ambalo limeonyesha kumkera kocha huyo raia wa Uingereza. 

Kerr amekerwa na hatua hiyo ya Simba kwa kuwa Kagere aliaga anarejea kwao Rwanda kushughulikia suala la pasi ya kusafiria, lakini akatua Dar es Salaam na kumalizana na Simba.


4 COMMENTS:

  1. Sasa anakererwa na nini? Kwani Kagere alikuwa bado anamkataba na Gor Mahia? Na kama hakuwa na mkataba walikuw wanasubiri nini kufanya nae mazungumzo?

    ReplyDelete
  2. siyo kazi ya kocha kuzuia usajili Gor wakiona mshiko mzuri wanaachia mchezaji na wewe salehe acha uyanga

    ReplyDelete
  3. Chukueni wote tu mtupunguzie mzigo Wa mechi yetu ya Shirikisho

    ReplyDelete
  4. Simba kimya kama vile wanasalimu amri na yale majigambo ya kwanza juwa hataituhusu Simba kuchukua ubingwa ujao sasa ni kimya au ndio mambo kimyakimya? Kishindo cha kumtaka Shiza Kichuya na Ndemla naona hakuna tena wanashindwa kuwapa mpya wamebakia kuwa Simba wanawahujumu na vipi wanahujumu na wachezaji wapo huru kwani wamesahau walovokuwa wakiwaonea Simba kuwachukuwa nyota wao kama vile unangoa jino bila ya kutia ganzi walimchukuwa yule Mrundi ambae Sumba wameshamlipa bila ya kuzirejesha kiyu ambacho kama eizi na sasa ndio Mungu analipa. Nayawayafike

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic