June 29, 2018



Wakati vuguvugu la usajili nchini Tanzania likishidi kushika hatamu haswa kwa klabu zinazoshiriki Ligi Kuu, imeelezwa kuwa Mshambuliaji Mbenin aliyekuja Yanga, Marcelin Koukpou, ameondoka na kuelekea kusikojulikana.


Awali uongozi wa Yanga ulisema Koukpou aliwasili nchini kuja kumalizana na Yanga lakini sasa inaelezwa mambo yamekwenda tofauti baada ya kuripotiwa kutimkia pasipojulikana huku Yanga wenyewe wakishindwa kuweka wazi ni wapi alipo.

Taarifa nyingine ambazo si rasmi zinaeleza kuwa Mbenin huyo aliyekuwa anaichezea Les Buffles FC ya Benin, amefeli mazoezi na pengine ndiyo sababu ya yeye kuondoka kwake.

Kiungo Mshambuliaji wa klabu ya Singida United, Dues Kaseke, ameanza kuhusishwa kurejea jijini Dar es Salaam kujiunga na timu yake ya zamani, Yanga, kabla ya msimu ujao wa ligi kuanza.

Kaseke ameingia kwa tetesi hizo ambapo awali ilielezwa kuwa ataondoka kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya kujiunga na klabu nyingine ambayo haikutajwa jina lake kwa ajili ya kusakata soka la kimataifa.

Uongozi wa Simba umesema bado haujafanya mazungumzo na kiungo wa Mtibwa Sugar FC, Hassan Dilunga ambaye amehusishwa kujiunga na mabingwa hao wapya wa ligi msimu wa 2017/18. 

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema kama watamuhitaji tuendelee kusubiri siku wakimtangaza kwani wao hawafanyi usajili wa kimakimya.



1 COMMENTS:

  1. Loo hata Mbenina kaingia mitini. Huenda slidokezwa kuwa wachezaji wengi wamegoma na hawataki kusaini mkataba mpya kutokana na kuanguka timu kipesa baada ya kukimbiwa na mfadhili wao na kukosa wachezaji wapya na wengine kugeuza usukani na kuelekea msimbazi na kuiomba Simba kulipiza kisasi kwa maovu waliyokuwa wakifanyiwa wakati wa enzi za Manji

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic