June 21, 2018


Real Madrid italazimika kumpatia hakikisho mshambuliaji Gareth Bale kuhusu muda atakaochezeshwa iwapo atasalia na mabingwa hao wa Ulaya msimu ujao, kulingana na ajenti wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28(Sky Sports)

Liverpool inatumai kumsajili mchezaji mwenye umri wa miaka 22 kutoka Aston Villa Jack Grealish huku Tottenham ikikataa kulipa dau la £20m kumnunua mchezaji huyo wa Uingereza wa kikosi cha wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 . (Sun)

Manchester United imeaambiwa wanaweza kumsajili beki wa Bayern Munich na Ujerumani Jerome Boateng 29 kwa dau la £50m. (Manchester Evening News)

West Ham inaendelea kuwa na matumaini ya kumsajili kwa dau la £35m winga wa Lazio na Brazil mwenye umri wa miaka 25 Felipe Anderson. (Telegraph)

Kiungo wa kati wa Uingereza Ruben Loftus-Cheek, 22, anasema kuwa atalazimika kuondoka Chelsea msimu huu ili kuweza kushirikishwa katika kikosi cha kwanza cha timu . (Mirror)

Everton inajiandaa kutoa £12m ili kumnunua mshambuliaji wa Hull City Jarrod Bowen, 22. (Sun)

Arsenal wamekamilisha dau la Yuro 30m kwa usajili wa kiungo wakati wa Sampdoria na Uruguay Lucas Torreira, 22, kulingana na rais wa klabu hiyo wa Serie A(TMW, via Evening Standard)

Mabingwa wa ligi kuu nchini Uingereza Manchester City wanatarajiwa kukamilisha uhamisho wa thamani ya £46.5m kumsajili kiungo wa kati wa Napoli na Italy Jorginho, 26 wiki hii. (Mirror)

Juventus itahitaji £70m kumsajili kiungo wa kati wa Bosnia mwenye umri wa miaka 27 Miralem Pjanic, abaye analengwa na Chelsea na Barcelona.(Corriere Dello Sport - in Italian)

Tottenham na Liverpool zinatarajiwa kumkosa winga wa Bordeaux Malcom huku Inter Milan ikikamilisha uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 kutoka Brazil (Sky Italia, via Talksport)

Mkufunzi wa klabu ya Rangers Steven Gerrard anatarajiwa kumsajili aliyekuwa mchezaji wa Liverpool Jon Flanagan, 25, katika uhamisho huru baada ya beki huyo wa kulia wa Uingereza kukamilisha ukaguzi wa kimatibabu. (Mail)

Newcastle inajaribu kumuuza kiungo wa kati wa Senegal 27 Henri Saivet kwa kklabu za Ulaya. (Chronicle)

Leicester City ina mpango wa kumnunua mshambuliaji wa Basel na Norway Mohamed Elyounoussi, 23, kuchukua mahala pake Riyadh Mahrez anayelengwa na Manchester City . (ESPN)

Real Madrid imewasajili wanawe mchezaji wa zamani wa Barcelona na Chelsea Eidur Gudjohnsen (Marca)

Kutoka BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic