June 29, 2018


Na George Mganga

Baada ya kuenea kwa tetesi kuwa kiungo wa Simba, Said Ndemla anaondoka ndani ya timu hiyo na ikielezwa kuwa anaweza akajiunga na watani zao wa jadi Yanga, uongozi umesema tayari wameshamalizana naye.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amefunguka na kueleza kuwa tayari wachezaji wote walio kwenye mipango na klabu wameshaboreshewa mikataba yao.

Manara ameeleza wachezaji ambao mikataba yao ilikuwa ukingoni wameshaongezewa na sasa wataendelea kutoa huduma ndani ya timu kwa misimu ujao na katika mashindano mbalimbali ambayo Simba inakabiliwa nayo usoni.

Wachezaji hao ni Mzamiru Yassin, Shiza Kichuya, Mohammed Ibrahim pamoja na Ndemla ambaye alianza kuhusishwa kuelekea Yanga.

Simba wamekamilisha dili za wachezaji hao ikiwa kesho wataanza rasmi kibarua cha michuano ya KAGAME kwa kucheza na Dakadaha ya Somalia kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 8 kamili mchana.

2 COMMENTS:

  1. Unaona mambo hsyo? Mwenye nguvu mpishe badalala ya kupiga pute sasa wao ndio wapigwao pute na wamebaki kutumbulia macho na kungoja rehema ya Mungu kama kishada kilichokata uzi hakijulikani kitaangukia wapi na huku majigambo kimya hakuna na Akilimali na Mkemia hawajulikani walipo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic