June 28, 2018


Ukiwa umesalia mwezi mmoja ujao kwa uongozi wa Simba uliopo madarakani kumaliza muda wake, Mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage, amesema hatoweza kugombea.

Rage ambaye aliweza kuiongoza Simba kabla ya utawala wa Evans Aveva kuingia madarakani, amesema yeye ni mwanachama na kwa sasa hana mipango tena ya kugombea nafasi ya Urais.

Kwa mujibu wa mazungumzo na Radio EFM, Rage ameeleza kuwa muda wake ulishamalizika na akiwatakia kheri Simba kuelekea uchaguzi huo mkuu wa klabu.

Ikumbukwe Rage aliiongoza Simba na kuweza kuiachia eneo la Uwanja uliopo Bunju ambao ndiyo kwenye mchakato wa kutengenezwa kwa ajili ya matumizi ya kikosi cha wekundu hao wa Msimbazi kwa hapo baadaye.

1 COMMENTS:

  1. uwanja wa bunju ulitafutwa chini ya uongozi wa dalali na kaduguda acheni upotoshaji

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic