June 3, 2018


Kikosi cha Singida United kimeondoka leo mjini Singida kuelekea Kenya kwa ajili ya kushiriki michuano ya SportPesa Super Cup inayoanza mjini Nakuru nchini humo.

Jumla ya wachezaji 20 wameondoka kuelekea Kenya ambapo Magolikipa ni Allya Mustapha Bathez, Peter Manyika Jr mabeki ni Miraji Adam, Shafik Batambuze, Kennedy Juma, Elisha Murouwa, Maliki Antiri, Salum Kipaga na Salum Chuku.

Viungo ni Nizar Khalifan, Kenn Ally, Deus Kaseke, Yusuph Kagoma, Elinywesia Sumbi, na Diaby Amara washambuliaji wapo, Lubinda Mundia, Danny Lyanga, Mbrazili Felipe Dos Santos, Tiber John na Habib Kyombo.

Wakati michuano hiyo ikianza leo kwa Yanga kukupiga na KK. Home Boys, Singida United wataanza kibarua chao cha kwanza dhidi ya AFC Leopards Jumanne ya June 5 2018.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic