June 22, 2018


Na George Mganga

Imeelezwa kuwa Mshambuliaji mpya wa Yanga kutoka Benin, Marcelin Koukpo tayari amefanyiwa vipimo vya afya na sasa yu tayari kuanza mazoezi na kikosi kuanzia wiki ijayo.

Taarifa zinaeleza kuwa Koukpo tayari alishawasili nchini muda mrefu na panapo majaaliwa wiki ijayo ataungana na wachezaji wenzake kuanza kujifua kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Daktari wa Yanga, Edward Bavu amekamilisha kumfanyia vipimo hivyo Koukpo ambaye alikuwa anaichezea Les Buffles ya nchini kwao kabla kujiunga na Yanga na kuonekana yupo fiti kiafya.

Koukpo tayari ameshamalizana na mabosi wa Yanga kupitia Mwenyekiti wa usajili, Hussein Nyika kwa kusaini mkataba wa miaka miwili.

Baada ya kukamilisha vipimo kwa mchezaji huyo, inaelezwa kuwa Yanga ipo kwenye mazungumzo na wachezaji wengine ikiwemo Mohamed Ibrahim wa Simba ambaye alikosekana katika michezo mingi ya msimu uliomalizika.

1 COMMENTS:

  1. Duuh, kaka una habari nyingi za kuokoteza zisizo na uhakika

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic