July 2, 2018


Klabu ya Arsenal imekamilisha usajili wa beki wa kati kutoka Borussia Dortmund, Sokratis Papastathopoulous . 

Papastathoulous amefikia makubaliano na mabosi wa Arsenal kwa kutia kandarasi ya mkataba wa muda mrefu uliogharimu kiasi cha euro milioni 20.

Mbali na Dortmund, beki huyo amewahi kuzichezea timu kubwa ikiwemo AC Milan, Werder Bremen, Genoa na AEK Athens.

Usajili wa Papastatholous umekuwa wa tatu kwa Kocha Unai Emery tangu atue klabuni hapo akichukua mikoba ya Arsene Wenger ikiwa ni baada ya kuwasaini Stephan Lichsteiner na Kipa Bernd Leno.

Emery amedhamiria kuieletea mabadiliko mapya Arsenal ikiwa ni maandalizi ya kukijenga zaidi kikosi hicho kuelekea msimu mpya ujao wa Ligi Kuu England na mashindano mengine.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic