BRAZIL YAZIDI KUWA TISHIO, YAWAPIGA MEXICO 2-0 NA KUTINGA ROBO FAINALI KOMBE LA DUNIA
Kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kimeendelea kucheka na nyavu baada ya kuiondosha Mexico katika hatua ya 16 ya Kombe la Dunia huko Urusi kwa kuifunga mabao 2-1.
Neymar Junior na Robeto Firmino ndiyo walikuwa chachu ya ushindi huo kwa kufanikiwa kuweka kimiani mabao hayo mawili na kuwafanya Brazil watinge hatua ya robo fainali.
Timu zote mbili zilimaliza dakika 45 za kwanza bila yoyote kutikisha nyavu lakini mnamo kipindi cha pili Brazil walirejea vizuri na kuweza kuandika mabao hayo yote mawili.
Baada ya mechi hiyo, baadaye saa 3 Ubelgiji watakuwa dimbani kukipiga dhidi ya Japan ikiwa ni hatua ya 16 bora pia.
0 COMMENTS:
Post a Comment