BAADA YA KUWAPIGA 4G DAKADAHA, SIMBA KUKIPIGA DHIDI YA APR LEO
Kikosi cha Simba kinashuka dimbani tena leo katika mashindano ya KAGAME kwa ajili ya kukipiga dhidi ya APR ya Rwanda.
Mchezo huo utakuwa wa pili kwa Simba baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Dakadaha ya Somalia katika mchezo wake wa kwanza.
Kuelekea mechi hii, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema wamejipanga vilivyo kuhakikisha timu inapata matokeo maana wanajua vizuri APR imepoteza mechi yake ya kwanza.
Simba wanaenda kukutana na APR ambayo ilipoteza mchezo wake wa kwanza kwa jumla ya mabao 2-1 dhidi ya Singida United kutoka Singida.
Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na wadau wengi wa soka la nyumbani na hata Afrika Mashariki itaanza majira ya saa 10 kamili jioni.
0 COMMENTS:
Post a Comment