BARAKAH DA PRINCE AAMUA KUBADILISHA DINI, SABABU AITAJA
Na George Mganga
Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Barakah Da Prince, ameamua kubadilisha jina na sasa atakuwa anaitwa AbdulMalik.
Kwa mujibu wa Baraka mwenyewe kupitia chombo cha habari (Clouds FM), amefunguka na kusema ameamua kufanya hivyo akiwashirikisha wazazi wake.
Baraka ameeleza maamuzi ya yeye kuamua kubadilisha dini kutoka Ukristo kwenda Uislam kuwa si kwasababu ya mwanamke aliye naye bali alikaa na kufikiria kisha kuwashirikisha wazazi wake.
"Sijabadilisha dini sababu ya mwanamke bali ni mimi mwenyewe nilikaa na kufikiria na nikawashirikisha familia yangu na walivyonipa baraka ikabidi nibadili" alisema Barakah.
Mwamuziki huyo amekuwa kwenye mahusiano na mwanamke wa kiislamu hivyo watu wengi wengi wamedai pengine ameshawishika kumfuata na kufikia uamuzi huo wa kubadili dini.
isiwe ishu sana ni mtu mzima huyo
ReplyDelete