July 3, 2018


Uongozi wa Real Madrid umekanusha taarifa zilizoripotiwa kuwa imetuma ofa kwenda PSG kwa ajili ya kumuhitaji nyota wake wa Kibrazil, Neymar Junior.

Hatua hiyo imefikiwa mara baada ya Madrid kuona taarifa hizo zinazidi kushika kasi kwenye vyombo tofauti vya habari Spain na Ufaransa mpaka imewabidi wazijibu kwa kuzikanusha.

Licha ya kukanusha taarifa hizo, Madrid wameanza kuhusishwa kwa muda mrefu kuhitaji saini ya mchezaji huyo aliyetoka Barcelona kwa kitita cha pauni milioni 198 kwenda PSG.

Mbali na tetesi hizo, Neymar aliripotiwa kuibuka na kueleza anajuta kujiunga na PSG huku ikielezwa alikuwa anahitahi kurejea tena Barcelona kuendelea na maisha ya soka.

Mchezaji huyo yuko nchini Urusi hivi sasa akiitumikia timu yake ya taifa ya Brazil na jana alichangia kuiwezesha kufika hatua ya robo fainali dhidi ya Mexico kwa kufunga bao moja katika ushindi wa 2-0.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic