July 3, 2018


Timu ya taifa ya Sweden imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Dunia huko Urusi kwa kufanikiwa kuifunga Uswisi bao 1-0.

Bao pekee la mchezo huo limewekwa kimiani na Emil Forsberg mnamo dakika ya 66 ya kipindi cha pili na kuweza kudumu kwa dakik zote 90.

Ushindi huo unaifanya Sweden iweze kuungana na timu za Ufaransa, Uruguay, Ubelgiji, Urusi, Croatia na Brazil ambazo tayari zimeshatinga hatua hiyo.

Safari ya 16 bora itahitimishwa baadaye kuanzia saa 3 kamili usiku ambapo England itakuwa kibaruani kucheza dhidi ya Colombia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic