Na George Mganga
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema kuwa klabu ya Mtibwa Sugar itaweza kushiriki mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika endapo italipa kiasi cha dola za kimarekani 15000.
Mbali kiasi hicho cha fedha, Mtibwa watapaswa pia kulipia gharama za safari ya klabu ya Santos ya Afrika Kusini kabla ya Julai 20 2018.
Ikumbukwe Mtibwa Sugar ilifungiwa na CAF kwa muda wa miaka mitatu kushiriki mashindano yake kutokana na kushindwa kupeleka timu Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo dhidi ya Santos.
Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao, amesema Mtibwa wanapaswa kuwajibika na gharama hizo za Santos pamoja na faini hiyo ili waweze kupata tiketi hiyo ya ushiriki wa mashindano hayo.
Mtibwa Sugar ilipata nafasi ya kuikwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuibuka bingwa wa kombe la FA dhidi ya Singida United kwa ushindi wa mabao 3-2 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
0 COMMENTS:
Post a Comment