BOSS AZAM AULA ARUSHA UNITED
Aliyekuwa Ofisa Mtendaji wa Azam FC, Saad Kawemba, amechaguliwa kuwa Mtendaji Mkuu kwenye klabu ya Arusha United iliyokuwa inajulikana kama JKT Oljoro hapo zamani.
Klabu hiyo ambayo ipo katika mchakato wa kuingia kwenye mfumo wa kampuni imeingia makubaliano na Kawemba kwa ajili ya kupata huduma yake kama mtendaji.
Kawemba ambaye aliwahi kuwa Azam, amesema kwa sasa wanajipanga kwa ajili ya kuijenga timu ili iweze kurejea kwenye ligi hapo baadaye.
Aidha, kiongozi huyo amesema kwa sasa wanaweka mikakati mizuri ili watoke kwenye mfumo wa kizamani na kwenda kisasa ili kuendana na wakati na kuiboresha zaidi Arusha United.
Timu ambayo inashiriki Ligi Daraja la kwanza itakuwa inapigania kurejea Ligi Kuu msimu wa 2019/18 baada ya msimu uliopita kushindwa kufanikiwa kurejea katika ligi.
0 COMMENTS:
Post a Comment