July 30, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Coastal Union ya Tanga umetangaza kuja kitofauti zaidi kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara utakaoanza Agosti 22 mwaka huu.

Ukiwa umesalia mwezi mmoja pekee kuelekea kufunguliwa kwa pazia hilo, Kocha wa timu hiyo, Juma Mgunda, amesema kuwa Coastal Union ya msimu ujao itakuwa na vijana lukuki.

Mgunda ameeleza kuwa vijana alionao ni bora na wana uwezo mkubwa wa kucheza mpira huku akizitumia salaam timu zote pinzani kuwa zijiandae kupokea dozi takatifu.

Mbali na kutumia zaidi vijana, Mgunda ameeleza pia juu ya usajili wa Msanii Alikiba ambaye ametia kandarasi ya mwaka mmoja kuwa yeye kama Kocha hataweza kumbania kazi zake za muziki.

Mgunda amefunguka na kueleza kuwa Kiba ni msanii wa kimataifa na jina lake ni kubwa hivyo kazi zake za muziki haziwezi zikazuiliwa na Coastal Union hivyo pale atakapokuwa anapaswa kufanya kazi zake hatokazwa.

Kauli hiyo imekuja kutokana na baadhi ya wadau ikiwemo mashabiki wa soka na muziku kuanza kuhoji kuwa inawezekana vipi Kiba akatimiza majukumu mawili kwa wakati mmoja huku akiimba na upande mwingine akicheza mpira.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic