July 30, 2018



Amissi Tambwe ambaye msimu uliopita hakufanya lolote ndani ya Yanga, amedai kwamba hatishwi na kambi ya Simba huko Uturuki wala uzoefu wa mastaa waliowasajili.

Tambwe ambaye habari zinadai amenusurika kutemwa na Yanga kutokana na hali mbaya ya kiuchumi ndani ya klabu hiyo amesema kwamba:-

“Kwa upande wetu wasitarajie mteremko maana mechi ambazo tunacheza sasa zinatujenga kwa kuirudisha miili yetu kwenye wakati wake kabla ya kuanza ligi.”

 “Tunajua tunacheza nao lini labda wao wanaweza pengine kujivunia wachezaji ambao wamewasajili lakini hata Yanga imesajili kwa ajili ya michuano yote kikubwa kwao wao na wajue tunafanya maandalizi ya kucheza na timu zote bila kujali walikuwa wapi katika maandalizi yao ya msimu kwa sababu tunajipanga kurejea kwenye nafasi yetu,” alisema Tambwe ambaye ni raia wa Burundi.

4 COMMENTS:

  1. Kama kweli Tambwe kaongea hivyo basi muflisi. Hana la maana la kuzungumza. Inawezekana wala yeye hajaongea.

    ReplyDelete
  2. Tambwe pambana upate namba kwanza. Wacha miguu ifanye kazi, mdomo uachie mihogo huko Jangwani

    ReplyDelete
  3. Unabeza nini wewe hali yako taabani umekosea kidogo tu kusekwa na nini wanachokifaidi yanga kutoka kwako ambapo umekuwa mzigo unayekula hela yao bila ya faida

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic