KIFARU AWAPA KITISHO SIMBA KUELEKEA NGAO YA HISANI, AWAPIGA KIJEMBE KWENDA UTURUKI
Msemaji wa klabu ya Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru, amewatumia salaam za moto Simba kuelekea mechi ya Ngao ya Hisani itakayopigwa jijini Mwanza katika Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Mechi hiyo itawakutanisha Mtibwa na Simba Agosti 12 2018 kutokana na kila mmoja kuondoka na kikombe katika msimu wa 2017/18 ambapo Mtibwa ametwaa kombe la FA na Simba akichukua taji la Ligi Kuu.
Kifaru amesema kuwa licha ya Simba kuweka kambi ya wiki mbili huko Uturuki, wao kama Mtibwa hawana wasiwasi dhidi ya kambi hiyo na akiwaambia wajiandae kuja kupokea kipigo pekee.
Kifaru ameeleza kitendo cha Simba kukimbilia Ulaya ni kama mbwembwe tu wala haiwapi tishia kwao kutokana na maandalizi ambayo wanazidi kuyafanya kwa sasa.
"Sisi tunawasubiria Agosti 12 pale CCM Kirumba Mwanza, hatuna wasiwasi na kambi yao ya Uturuki kwa maana haitawasaidia kitu. Wajiandae kupokea kichapo tu kwa maana kikosi chetu kinajiandaa kisawasawa" alisema.
Domo jumba ya maneno, kasema Mhindi
ReplyDelete