DILUNGA AWAJIBU YANGA BAADA YA KUANZA KUMTAKA UPYA
Kiungo aliyewahi kupigwa chini na Yanga kwa madai kwamba amechuja, akatua Mtibwa Sugar na kung’ara, Hassan Dilunga yuko tayari kurudi Jangwani.
Kwa mujibu wa gazeti la Spoti Xtra, mchezaji huyo bora wa mashindano ya Kombe la FA, amesema kuwa ni jambo la furaha sana kwake kutakiwa na timu kubwa kama Siginda United na Yanga.
“Kwangu mimi ni jambo la faraja kuwa na mazungumzo na timu za Ligi Kuu hivyo sina mashaka na hilo kwani kazi yangu mimi ni mchezaji na ninapohitajika kutumikia timu nyingine maana kuna kitu cha pekee ambacho timu inayohitaji huduma yangu imekiona hivyo sina chaguo na kazi.
“Timu zote ambazo nimekuwa nikihusishwa kujiunga nazo ambazo ni pamoja na Yanga, Singida United nimewaweka wazi kwamba nina mkataba na timu yangu ya Mtibwa hivyo kama kweli wanahitaji huduma yangu wazungumze na uongozi kisha nami nitasaini kwa timu yoyote ambayo itakuwa ina maslahi mazuri kwangu,” alisema Dilunga ambaye amewahi kucheza JKT Ruvu.
This comment has been removed by the author.
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteMPIRA WA TANZANIA UNAKUFA KWANI BILA YA YANGA BORA SOKA LA TAIFA LITADIDIMIA KWANI MAPATO YA UWANJANI YATASHUKA, MSISIMKO WA SOKA UTAPUNGUA. KUNA HATARI KUBWA KWA VIONGOZI WA YANGA WANAOHUSIKA NA USAJILI MBOVU IKIWAMO KUDAIWA KUTAKA 10% KUVAMIWA NA KUDHURIWA NA HATA KUPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA HASIRA NA JAZBA ZA WAPENZI. KUNA WATANZANIA HIVI SASA WANA HASIRA SANA KWA JINSI MAMBO YANAVYOENDA MSIFIKIRI WANAFURAHIA....HII AMANI ITATOWEKA. CHONDE CHONDE NAOMBA TUSIFIKE HUKO, WADAU INUSURUNI YANGA KWA KUMALIZA SUALA LA USAJILI BORA TOENI FEDHA!
ReplyDeleteMbona mlisema anatakiwa na Simba nyie waandishi mbona wachonganishi sana, mnaandika habari kiushabiki mno...hamzingatii maadili ya kazi. Mnaiua tasnia ya michezo
ReplyDelete