Katika mchezo huo ambao Simba walikuwa na wachezaji takribani wote wa kikosi cha pili, uliwang'arisha vijana ambao waliongozwa na mkongwe wao Mwinyi Kazimoto Uwanjani.
Katika safu ya ushambuliaji, Simba ilikuwa na Adam Salamba, Juma Rashidi na Moses Kitandu wakati huo Marcel Kaheza naye akitumika kuwalisha mipira washambuliaji wa mwisho akicheza kama kiungo mshambuliaji.
Adam Salamba, aliweza kuifungia Simba mabao mawili na kuweza kuandika rekodi yake kuifungia klabu hiyo kongwe katika mchezo wake wa kwanza kwenye Uwanja wa Uhuru.
Uwepo wa wachezaji hao unaleta taswira mpya ya kikosi cha Simba ambacho kinaweza kuwa tishio baadaye endapo vijana hao wataendelea na kasi waliyoanza nayo.
Kikosi hicho pia kilipewa nafasi katika mashindano ya SportPesa huko Kenya japo hakikuweza kufanya vizuri kutokana na kutokuwa kambini kwa mrefu suala lililosababisha kukosa muunganiko mzuri.
Yawezekana ikawa ni mapema zaidi kukipa kipimo dhidi ya Dakadaha walioonekana kuwa dhaifu, tujaribu kukiangalia kwenye michezo mingine kwa kuwa bado mashindano yanaendelea.
Siku njema inaonekan asubuhi
ReplyDelete