July 1, 2018


Beki mpya wa Simba, Pascal Wawa ameweka wazi licha ya kudaiwa ni mhenga kwake haiwezi kumsumbua kwani amejipanga kutumia uzoefu wake wote kwa kuhakikisha timu hiyo inabeba Kombe la Kagame.

Raia huyo wa Ivory Cost ambaye amejiunga na Simba kwa mkataba wa mwaka moja akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na El Merrekh ya Sudan ambapo atacheza michuano hiyo kwa mara yake ya pili baada ya mwaka 2015 kufanikiwa kuipa ubingwa wa kombe hilo, Azam FC kabla ya kutimkia Sudan.

Wawa ambaye aliiponyoka Yanga dakika za mwisho ilipokuwa ikiwaza kumtumia tiketi ya ndege, alisema ; “Binafsi kwangu ni jambo la furaha nimerejea Tanzania kwa mara nyingine ila sasa nikiwa Simba tena naanza kazi katika michuano ya Kagame ambayo
nilihusika katika ubingwa wake wa mwisho wakati nipo Azam ingawa siwezi kuwaongelea.”

“Kikubwa nitahakikisha natoa uzoefu wangu wote kwa wenzangu kuhakikisha wote tunafikia malengo katika haya mashindano kwa sababu najua ugumu na ushindani wake ulivyo na ukiangalia bado anacheza na wachezaji ambao ni wageni kwangu sasa lazima nifanye kitu kama hicho ili watu waone tofauti na siyo kuangalia umri wangu upoje,” alisema Wawa mwenye miaka 32.

Beki hiyo tangu ameanza mazoezi na kikosi hicho amekuwa akitumia muda mwingi kutoa maelekezo kwa wachezaji wenzake anaocheza nao katika safu ya ulinzi kwa sasa ambao ni Paul Bukaba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na Ally Shomari kwa kuhakikisha wanafanya kazi yao vizuri.

CHANZO: SPOTI XTRA

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic