July 31, 2018


Mambo ni hivi! Familia ya staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ imesusia mwaliko wa bethidei wa mwanamitindo Hamisa Mobeto ambaye ni mzazi mwenza na msanii huyo.

Familia hiyo inadaiwa kususia mwaliko huo ambao ni wa bethidei ya mtoto wa Mobeto, Abdul Nasibu ‘Dylan’ aliyezaa na Diamond lakini imekuwa bize zaidi na maandalizi ya sherehe ya bethidei ya Tiffah aliyezaa na mjasiriamali, Zarinah Hassan ‘Zari’ anayeishi nchini Afrika Kusini.

Shamrashamra za sherehe ya Tiffah zimekuwa gumzo kwa takriban majuma matatu sasa, huku familia ya Diamond ikieleza wazi kuwa inajipanga kwenda Afrika Kusini kushiriki kikamilifu.

Chanzo makini kilieleza kwamba familia ya Diamond imegomea kwenda kwenye bethidei inayoandaliwa na Mobeto kwa ajili ya Dylan ambaye pia ni mtoto wa mwanamuziki huyo inayotarajiwa kufanyika Agosti 7, mwaka huu.

“Unaambiwa familia ya Diamond haitaki kusikia mtu anayeitwa Mobeto maana hawampendi hivyo licha ya kwamba Dylan amezaliwa mwezi mmoja na Tiffah lakini wao wako upande mmoja wa Tiffah,”kilieleza chanzo.

NDUGU AFUNGUKA

Akizungumza na Wikienda, dada wa mwanamuziki huyo Esma Khan, alisema kuwa hawezi kwenda kwenye bethidei hiyo kwa sababu hawajawahi kualikwa kwenye sherehe zao hata siku moja, hivyo hawawezi kwenda wala hawatarajii kusogea.

“Hivi ushawahi kuona klina Hamisa wanatualika kwenye ishu zao hata kidogo? Hivyo hatuwezi kwenda hata kidogo wala hatutarajii kabisa,” alisema Esma.

Ndugu mwingine ambaye yuko karibu na familia hiyo alisema kuwa hakuna sababu ya kufichaficha kwa kuwa hakuna ambaye ana mpango wa kwenda kwenye sherehe hiyo maana wao akili yao ipo Sauzi tu kwenye sherehe ya Tiffah.

“Hapa sisi akili yetu ni huko Sauzi tu kwenye bethidei ya Tiffah, huko kwingine hatuna mpango wa kwenda kabisa,” alisikika ndugu huyo akisema.

Kumekuwa na sitofahamu kuhusu sherehe hizo mbili za watoto wa Diamond, huku kila mmoja akijiuliza mbona inayosikika ni bethidei ya Tiffah na siyo Dylan ambaye pia ni mtoto wa Diamond.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic