YANGA WATHIBITISHA KUPATA KWA KIBALI CHA ZAHERA, DODOMA YATAJWA KUCHELEWESHA MIPANGO
Baada ya kuwakosa tena Gor Mahia akiutazama mchezo wa mkondo wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika akiwa jukwaani, uongozi wa klabu ya Yanga umesema kuwa kocha wake, Mwinyi Zahera tayari ameshapata vibali.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano kupitia Radio EFM, Hussein Nyika, amefunguka na kueleza sababu za Zahera kushindwa kuwa katika sehemu ya benchi la ufundi katika mechi dhidi ya Gor Mahia ilikuwa ni vibali vya kazi kukosekana.
Nyika ameeleza ofisi nyingi za serikali kuhamishiwa Dodoma hivi sasa ni zimechangia mchakato wa kupata vibali vyake kuwa mrefu hivyo kupelekea kuchelewa kutokana na umbali uliopo baina ya jiji hilo na Dar es Salaam.
Mbali na Dodoma, Nyika amesema pia kwa namna Yanga na kipindi hiki inachokipitia kumekuwa na mambo mengi ambayo yamekuwa yakikinzana na mipango ya klabu hivyo pia imepelekea kibali cha Mkongomani huyo kuzidi kuchelewa.
Lakini sasa Nyika amethibitisha vibali vya Zahera tayari vimeshapatikana na atakuwa anaonekana kwenye benchi la ufundi Yanga baada ya mambo kwenda sawa na kila kitu kimekamilika juu ya kibali cha kufanyia kazi.
Sasa tutarajie ushindi baada ya ushindi mpaka kumaliza mechi zilizobakia na mwishoni ubingwa kwasababu kila kitu kimeshatimia na hakuna kilichopunguwa
ReplyDeleteAngalau
ReplyDeleteHAKUNA KOCHA HAPO......UTAKATAAJE WACHEZAJI WA KUSAJILIWA AMBAO UNAPEWA BURE HUKU HALI UNAJUA KUWA KLABU IN A MAPUNGUFU YA BEKI WA KATI NA NAMBA 2, HALAFU UNAPEWA BEKI MZIMBABWE BURE UNAMKATAA, HE BEKI MMOJA KATI YA WALIOPO AKIUMIA UTAFANYA NINI? KOCHA ASIYEITAKIA TIMU MEMA HUYU. PIA UNAJUA KUWA TIMU IN A MAPUNGUFU YA STRAIKA NAMBA 9, 10, LAKINI UNASAJILI STRAIKA MMOJA TU, HUYU SI KOCHA MWENYE KUITAKIA MEMA TIMU. HALAFU HANA KIWANGO. YANGA SHUTUKENI MAPEMA!
ReplyDeleteKocha ana nafasi kubwa ya kuimarisha viwango vya wachezaji kwa maoni yangu vimeshuka, lakini pia kufanya kazi bila vibali kunashusha kujiamini (confidence). Tumpe muda afanye kazi halafu tumpe tuzo hasi au chanya.
ReplyDeleteWatu hawadanganywi siku hizi, ukweli uko wazi, huyo Mwinyi Zahera sio kocha atakayeleta mabadiliko chanya. Usajili wa timu ya Yanga kwa msimu wa 2018/2019 ni mbovu sana....halafu cha ajabu Kocha huyu au wakina Nyika wanakataa msaada wa wachezaji ambao wanakuja kuziba mapengo na mapungufu. Kocha atafukuzwa baada ya mechi 5 tu, benchi lote la ufundi linavunjwa, na usajili mdogo unafanyika ili kurudisha imani ya mashabiki iliyopotea, ambayo imepelekea kufanya wapenzi wa Yanga wasihudhurie mechi. Watu wamedanganywa sana sasa wamegundua uongo wote na ndio maana hawatoi ushirikiano na support. Kocha aliyeletwa ni mbabaishaji, timu haina mbinu za kiufundi wala haionyeshi iko fiti kimashindano, ukijumlisha na ubovu wa aina ya wachezaji waliopo basi ni sheeda 😁😁😁

ReplyDelete