July 1, 2018


Imeripotiwa kuwa beki wa kushoto wa klabu ya Yanga, Haji Mwinyi, amefunguka na kueleza kuwa kikosi chao kitafanya maajabu kwenye michuano ya CAF tofauti na wengi wanavyodhania.

Kikosi cha Yanga kipo chimbo kambini hivi sasa kikijiwinda kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia FC utakaopigwa Julai 18 kwenye Uwanja wa Machakos jijini Nairobi Kenya.

Taarifa zimeeleza Mwinyi amesema kuwa licha ya klabu hiyo kupitia wakati mgumu kwa sasa ikiwemo suala la kyumba kwa uchumi, si sababu ya wao kufana vibaya kuelekea mechi hiyo kubwa.

Mwinyi anaamini uwepo wa Kocha wao mpya, Mkongomani, Mwinyi Zahera utawapa nguvu ya kupambana zaidi dhidi ya mabingwa hao watetezi wa Kenya kwenye mtanange huo wa mkondo wa kwanza huko Nairobi.

Ikumbukwe Yanga haijapata ushindi wowote mpaka sasa katika kundi walilopangwa zaidi ya kupoteza 4-0 dhidi ya MC Alger, suluhu dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda na mchezo ujao watacheza ugenini na Gor Mahia.

Kauli hiyo ya Mwinyi inakuwa kama inawapiga mkwara MC Alger ambao watakuja Tanzania kurudiana na Yanga pamoja na Gor Mahia watakayokutana nayo hivi karibuni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic