Wakati mpaka sasa ikiwa haijajulikana juu ya timu ambayo Simba itacheza nayo katika tamasha lake la Simba Day, Ofisa wa Habari wa klabu hiyo, Haji Manara, amefunguka na kuweza wazi jambo hilo.
Manara ameeleza kuwa hivi sasa ni mapema sana kuitaja timu watakayocheza nayo kwani bado nguvu zao zipo katika maandalizi ya msimu ujao ambapo timu imeweka kambi Uturuki.
Manara amesema kuelekea tarehe 2 mpaka 3 Agosti timu hiyo itawekwa wazi lakini kwa sasa haiwezi kutajwa akieleza kuwa wakati mwafaka haujawadia.
Aidha, Manara amesema Simba inaendelea vema na mazoezi huko Uturuki ambapo kila hali ya mchezaji kiafya ipo salama na hakuna aliye majeruhi kwa wakati huu.
Kikosi hicho kimekuwa kikijifua kimazoezi ndani ya Uwanja na nje kwa maana ya kwenda gym kwa lengo la kuwapa wachezaji nguvu ya kuwapa stamina pindi wanapokuwa mchezoni.
0 COMMENTS:
Post a Comment