July 30, 2018


Kikosi cha Simba kinaendelea na mazoezi katika Milima ya Kartepe huko Uturuki kwa ajili ya maandalizi ya tamasha lake la Simba Day ambalo hufanyika kila mwaka Agosti 8.

Katika mazoezi hayo ambayo yapo chini ya Kocha Mkuu, Mbelgiji, Patrick Aussems, amewaamuliwa haswa wachezaji wake kwa kuwapa tizi mara mbili kwa siku.

Kocha huyo ameamua kufanya hivyo ili kuwafanya wawe na pumzi ya kutosha kwa ajili ya kuweza kuja kuhimili mikimiki ya msimu ujao katika ligi na mashindano ya kimataifa.

Wakati timu ikiendelea kujifua kwa kufanya mazoezi mara mbili kwa siku, kikosi hicho kinatarajiwa kuanza safari ya kurejea nchini Agosti 4 2018.

Simba itarudi nchini tayari kwa kukamilisha maandalizi ya tamasha la Simba Day na pia mchezo wa Ngao ya Hisani dhidi ya Mtibwa Sugar FC.

2 COMMENTS:

  1. Agosti 18???? Mwandishi mbona hauko makini? Ni Agosti 8

    ReplyDelete
    Replies
    1. macho yako kama yana matege..ni wapi pameandikwa August 18???????

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic