JKU YAIBUKA KIDEDEA DHIDI YA KATOR, YAITANDIKA 2-0
Klabu ya JKU imepata ushindi wake wa kwanza katika mashindano ya KAGAME kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kator kutoka Sudan Kusini.
JKU wamekubali kurekebisha makosa yao baada ya mechi ya kwanza kwenda sare ya 1-1 dhidi ya Vipers SC kutoka Uganda.
Baada ya mchezo huo kumalizika, baadaye kuanzia saa 2 usiku mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Azam FC watakuwa wanacheza dhidi ya Vipers.
MIkumbukwe katika mchezo wa kwanza Azam iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya APR.
0 COMMENTS:
Post a Comment