HARRY KANE APINDUA MEZA KIBABE URUSI DHIDI YA COLOMBIA
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya England, Harry Kane, jana alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mechi dhidi ya Colombia katika mchezo wa Kombe la Dunia nchini Russia.
Kane aliisaidia timu yake kufunga bao ndani ya dakika 90 huku akifunga pia katika hatua ya upigaji wa mikwaju ya penati baada ya dakika 120 kumalizika.
Katika mchezo huo, England ilifanikiwa kutinga hatua ya roo fainali kwa ushindi wa mabao 4-3 yaliyopatikana kwa upigwaji wa matuta baada ya dakika 90 kwenda sare ya 1-1.
Hatua inayosubiriwa hivi sasa ni ile ya robo fainali ambapo jana Colombia na England walikamilisha 16 bora.
0 COMMENTS:
Post a Comment