July 4, 2018


Imeripotiwa kuwa straika aliyewahi kusajiliwa na mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Simba SC, Dan Sserunkuma, ameibuka na kueleza sababu iliyomfanya akaondolewa Simba.

Sserunkuma ambaye alisajiliwa na wekundu wa Msimbazi akitokea katika klabu ya Gor Mahia ya Kenya, amesema viongozi wachezaji wengi hawapewi nafasi.

Mchezaji huyo ambaye yupo hapa nchini na Vipers FC ya Uganda kwa ajili ya kushiriki mashindano ya KAGAME, amefunguka na kueleza kuwa viongozi wengi wanakosa ushirikiano na wachezaji wa kigeni.

Aidha, Ssserunkuma ameeleza kuwa hajajua sababu inayowapelekea kufanya hivyo ni nini mpaka akasitishiwa mkataba wake baada ya miezi 6 kumalizika na kuamua kuelekeaUganda.

Straika huyo ameifungia Vipers mabao mawili katika mechi mbili ambazo Vipers imeshacheza mpaka sasa ambapo amefunga dhidi ya JKU ya Zanzibar na Azam FC.


3 COMMENTS:

  1. Sasa fitina za viongozi walookuwa wakiidhuru Simba kwa maslahi yao hawana lao na hawapo na wala hawatarehea wala hawatorejea. Simba imetulia na inaendeshwa na wanaoionea uchungu

    ReplyDelete
  2. Huyu nae hana lolote sasa alitaka viongozi waingie uwanjani wakamfanyie assist goli? Mchezaji wa ukweli hana longolongo nyingi za maneno huonyesha maneno yake kwa vitendo uwanjani.

    ReplyDelete
  3. mpira ulimkataa Tanzania asichonganishe viongozi, mashabiki walijitahidi sana kumpa support tangu day one yeye akawa ananenepeana tu, najiuliza kama hata Mavugo ataongea hivi pam0ja na support yote ya washabiki yeye anakimbizana na ngono tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic