NI VITA YA SIMBA NA SINGIDA UNITED TAIFA LEO
Na George Mganga
Vita kubwa ya michuano ya KAGAME inaendelea leo kwenye Uwanja wa Taifa ambapo Simba watakuwa wanacheza dhidi ya Singida United.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali kutokana na Singida United haijawahi kupata matokeo mbele ya Simba tangu ipande daraja kushiriki Ligi Kuu Bara.
Katika mechi zote mbili zilizopita za ligi, Singida ilikubali kupoteza alama tatu hivyo mchezo wa leo unaweza ukawa wa kulipiza kisasi.
Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na wadau wa soka Tanzania, itaanza majira ya saa 10 kamili jioni.
Tayari timu zote jana zimefanya maandalizi ya kujinoa vilivyo kuelekea mchezo huo ambao Singida watakuwa wanacheza na Simba kwa mara ya kwanza katika michuano hiyo ya KAGAME>
0 COMMENTS:
Post a Comment