SIMBA WANOA SILAHA ZAO TENA KWA AJILI YA KAZI MAALUM KESHO DHIDI YA APR
Kikosi cha Simba kimeendelea na mazoezi katika Uwanja wa Boko Veterani leo kwa ajili ya maandalizi kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya APR.
Simba watakuwa wancheza mechi hiyo ya pili baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Dakadaha FC ya Somalia katika mchezo wao wa kwanza.
Ikumbukwe APR itakuwa inaingia kusaka matokeo baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Azam kwa jumla ya mabao 2-1.
Kuelekea mechi ya kesho, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema kwa wanaiheshimu APR na wamejipanga kupambana kwa ajili ya kusaka ushindi.
Mechi hiyo itachezwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
0 COMMENTS:
Post a Comment