July 31, 2018


Straika mpya wa klabu ya Azam FC, ameanza mazoezi huko Uganda ambapo timu hiyo imeweka kambi ya wiki mbili.

Ngoma ameanza mazoezi mepesi kufuatua ushauri wa daktari wake juu majeruhi aliyonayo ili kujiweka fiti taratibu kuelekea dirisha la ligi kufunguliwa Agosti 22.

Ikimbukwe nGoma alipewa mapumziko ya wiki tisa baada ya kugundulika ana uvimbe kwenye goti lake la kulia ikiwa ni baada ya kufanyiwa vipimo vya afya katika hospitali ya St. Vincent Parrot iliyoko Afrika Kusini.

Taarifa kutoka Azam zinaeleza hali ya Ngoma kwa sasa inaendelea vizuri japo bado hajaimarika kisawasawa ingawa matumanini ya kupona kwake yapo kwa siku za usoni.

Azam inatarajiwa kurejea nchini baada ya wiki ijayo tayari kwa maandalizi ya mwisho kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.

2 COMMENTS:

  1. Aaah au baada ya kuombewa na TB Joshua?

    ReplyDelete
  2. Ndio baada ya kumwagiwa maji ya uzima tunguli peke yake hazikutosha.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic