LEBRON ASAINI BN. 350/= KUJIUNGA NA LOS ANGELES LAKERS
Mfalme wa ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani, LeBron James, amesaini kujiunga na timu ya Los Angeles Lakers kwa kitita cha Dola 154 ambazo ni sasa na Sh. bn. 350 za Tanzania.
Taarifa ya shirika la Klutch Sports linalomwakilisha Bron, ilisema nyota huyo amesaini mkataba wa miaka minne na timu hiyo ya mchezaji wa zamani wa mchezo huo, Magic Johnson.
Inasemekana mchezaji huyo ambaye anategemewa kutangaza kujiunga na timu hiyo kesho (Jumanne), huenda akaungana na mchezaji mwingine mpya wa timu hiyo, Kawhi Leonard, kutoka timu ya San Antonio Spurs.
0 COMMENTS:
Post a Comment