SALAH AZIMA NDOTO ZA MADRID, ASAINI MKATABA WA MUDA MREFU NA LIVERPOOL
Mchezaji bora wa Ligi Kuu England katika msimu wa 2017/18 Mohamed Salah, ameisaini mkataba wa muda mrefu kuendelea kuitumikia klabu ya Liverpool.
Salah amefikia makubaliano na mabosi wa Liverpool kuongeza muda wa soka la maisha yake na timu hiyo na kuzima rasmi tetezi za kuondoka Anfield.
Mshambuliaji huyo kutoka taifa la Misri, atakuwa anatengeneza rekodi ya kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi ndani ya klabu hiyo, kiasi cha pauni milioni 200,000 kwa wiki.
Kabla ya kusaini mkataba huo, Salah alianza kuhusishwa kuelekea Real Madrid kwa ajili ya kusajiliwa na mabingwa hao wa kihistoria Real Madrid lakini amezima uvumi huo na sasa atasalia Liverpool mpaka mwaka 2023.
0 COMMENTS:
Post a Comment