LICHA YA KUELEZWA AMEFELI MAZOEZI, AZAM WAFUNGUKA KIVINGINE JUU YA ZAYD
Baada ya kuelezwa kuwa amefeli mazoezi huko Afrika Kusini katika klabu ya Bidvest Wits, uongozi wa Azam FC umesema kuwa mchezaji Yahya Zayd amerejeshwa kwa muda.
Kinda huyo alielekea katika klabu hiyo na kupewa muda wa wiki mbili ya kufanya majiribio lakini badala yake amekaa kwa wiki moja pekee na kurejeshwa nchini.
Taarifa kutoka Azam zimeleeza kuwa klabu ya Bidvest Wits imemrejesha mara moja Zayd na baadaye watamuita tena kwa ajili ya kuendelea na majaribio kwa mara ya pili ili kuweza kuona kama atafaulu au la.
Wakati Zayd akirejeswa Tanzania, kikosi cha Azam kimeondoka nchini juzi kuelekea Uganda kwa ajili ya kambi maalum kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.
Azam wameondoka huku kikosi kikiwa chini ya Kocha Mholanzi, Hans van der Plujim ambaye alikuwa Singida United msimu uliopita tayari kuwanoa wachezaji wake kwa msimu mpya utakaoanza Agosti 22.
0 COMMENTS:
Post a Comment