July 31, 2018


Na George Mganga

Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah (Try Again), amefunguka kuhusiana na kuchelewa kuripoti kwa kiungo wao, Mrwanda, Haruna Niyonzima katika klabu hiyo baada ya likizo kumalizika.

Abdallah amesema kuwa mpaka sasa wao kama viongozi hawaelewi kipi kimesababisha mchezaji huyo kushindwa kuwasili nchini ambapo alipaswa kurejea mapema ili aweze kusafiri kuelekea Uturuki.

Niyonzima alipaswa kurejea nchini ili aweze kusafiri na wachezaji ambao ni Said Ndemla, Meddie Kagere, Erasto Nyoni na Hassan Dilunga ambao walichelewa kutokana na viza zao kutokamilika mapema.

Kwa mujibu wa Radio One kupitia Spoti Leo, Abdallah ameeleza kwa sasa hawana lolote ka kuhukumu na badala yake wanasubiri utetezi wake ili kujua kipi kilikuwa kinamsumbua na kama kuna adhabu wataitoa dhidi yake.

"Likizo ya Haruna Niyonzima ilimalizika tangu July 20, lakini mpaka sasa kama uongozi hatuelewi tatizo gani limemtokea mpaka kupeleka kuchelewa kuwasili nchini hadi leo.

"Tutampa nafasi ya kumsikiliza kwasababu hatuwezi kutoa hukumu kabla ya kujua tatizo lake ni lipi, na kuhusu kwenda Uturuki kwa sasa haitowezekana kwasababu tayari yupo nje ya muda" alisema.

Hata hivyo Abdallah amemsifia Niyonzima na kusema kuwa ni moja kati ya wachezaji wazuri wenye uwezo mkubwa uwanjani ingawa msimu uliopita hakuwa vizuri kutokana na kusumbuliwa na majeraha.


2 COMMENTS:

  1. Sidhani kama atapata namba kikosi cha kwanza. Tangu akiwa Yanga hajawahi kuheshimu muda. Kipaji bila nidhamu ni bure tu.

    ReplyDelete
  2. Niyomiza ni binaadamu na inawezekana akawa na matatizo fulani, lakini kiungwana alibidi kuujuilisha uwongozi. Ukirejea nyuma huyu kijana sio mara yake ya kwanza kuyatenda hayo. Miaka ya nyuma aliyatenda kama hayo alipokuwa katika kikosi cha yanga na nakumbuka ilifika hadi timu yake ilikuwa tayari kuachana naye lakini alipofika, akaangukia miguu kwa maandishi na akasamehewa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic