LICHA YA KUTUPWA NJE KOMBE LA DUNIA, UJERUMANI YAMWONGEZEA MKATABA MREFU KOCHA WAKE
Licha ya kuondoshwa katika fainali za michuano ya Kombe la Dunia Urusi, uongozi wa timu ya taifa la Ujerumani umezidi kumwamini Kocha wake Joachim Low kwa kumuongezea mkataba mwingine.
Low amefikia makubaliano na mabosi wake kwa kukubali kutia kandarasi ambapo sasa atakuwa na timu hiyo mpaka mwaka 2022.
Low hakuweza kufanya vema kwenye mashindano hayo mwaka huu kwa timu yake kutolewa kwenye hatua ya makundi na Korea Kusini kwa mabao 2-0.
Kichapo hicho hakijaweka kumuweka kando Kocha huyo kutokana na kuaminiwa kwake suala lililowapelekea viongozi wa ngazi za juu kufanya naye mazungumzo ya kuongeza mkataba mwingine.
0 COMMENTS:
Post a Comment