July 3, 2018


Kikosi cha Singida United kesho kitakuwa na kibarua kizito cha kulipiza kisasi dhidi ya Simba katika mchezo wa Kombe la KAGAME utakaopigwa Uwanja wa Taifa.

Rekodi zinasema Simba haijawahi kufungwa na Singida tangu walima alizeti hao kutoka Singida wapande kushiriki Ligi Kuu Bara.

Katika mechi ya kwanza iliyowakutanisha Simba na Singida Januari 18 2018 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam walikubaki kipigo cha mabao 4-0 ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu.

Na katika mchezo wa mzunguko wa pili Singida United wakiwa kwenye Uwanja wa Namfua walikubali pia kichapo cha bao 1-0 hivyo kuzidi kujiwekea rekodi mbovu dhidi ya Simba.

Kesho majira ya saa 10 kamili jioni watakuwa wanakutana mara ya tatu kwenye Uwanja wa Taifa wakiwa na kumbukumbu ya kile kichapo cha mabao 4-0 walichokipata kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic