WACHEZAJI TIMU YA TAIFA WALALA MTAANI
Wachezaji wa timu ya taifa ya rugby ya Zimbabwe wamelazimika kulala mitaani nchini Tunisia wakisubiri mechi yao mwishoni mwa wiki hii.
Hali hiyo imesababishwa na hali mbaya ya kifedha na kuifanya timu hiyo iliyo chini ya kocha Peter de Villiers, kulala mitaani.
Zimbabwe ilifungwa 45-36 na Kenya katika michuano ya awali ya kuwania kushiriki Kombe la Dunia la Rugby iliyofanyika wiki iliyopita nchini humo.
Habari zinasema timu hiyo ilizuiwa uwanja wa ndege kwa kushindwa kulipia ‘visa’ za kuingia nchini humo ambapo wachezaji walikuwa hawakulipwa chochote walipokuwa nchini Kenya.
Kuhusu chakula, inasemekana kocha De Villiers ndiye aliwanunulia kwa fedha yake binafsi.
Imeandaliwa na Global Publishers
0 COMMENTS:
Post a Comment