MAHREZ NA MAN CITY SASA MAMBO SAFI, LEICESTER YAKUBALI YAISHE
Imeripotiwa kuwa winga wa Leicester City, Riyad Mahrez yuko mbioni kukamilisha uhamisho wake kuelekea Manchester City.
Mahrez amekuwa akiwindwa kwa muda mrefu na Kocha Pep Guardiola japo mabosi wa Leicester walikuwa wakitia ngumu kumuachia.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka vyanzo mbalimbali barani Ulaya vimeeleza Man City na Leicester wamefikia patamu na mchezaji huyo anaweza akawasili Manchester kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya.
Mahrez ambaye yupo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Algeria, alifanikiwa kufunga jumla ya mabao 13 katika michezo 41 ya Ligi Kuu England msimu uliopita.
0 COMMENTS:
Post a Comment