July 30, 2018



Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ameonyesha imani yake kubwa kwa beki wake, Kelvin Yondani baada ya kumkataa beki wa  Singida United, Elisha  Muroiwa ambaye alitarajiwa kutua klabuni hapo.

Yondani ndiye mchezaji wa mwisho aliyesajiliwa Yanga ambapo usajili wake uliokamilika saa 5:00 usiku wa kuamkia Ijumaa iliyopita ikiwa imebakia saa moja kabla kufungwa dirisha la usajili kufuatia matakwa ya Zahera ambaye aligomea kutua kwa beki huyo wa Singida.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Yanga, Hussein Nyika amesema, Zahera hakukubaliana na kiwango cha Muroiwa kwa madai kuwa kiwango cha Yondani ni kizuri zaidi ya beki huyo hivyo uwepo wake katika timu hiyo utasaidia kuifanya timu yake iweze kuwa vizuri msimu ujao.

“Mwalimu alivyomuona Muroiwa alieleza wazi kwamba, kiwango chake hakiwezi kumchalenji Yondani na kusema kuwa kiwango cha Yondani ni kizuri hivyo beki yeyote anayetakiwa kutua Yanga awe na kiwango cha kumzidi na si vinginevyo. 

“Mwalimu alikuwa akimuhitaji Yondani kwa hali na mali na ndiyo maana tulijitahidi kuhakikisha anabaki katika dakika za mwisho na alipobaki tu hakuwa na haja tena na Muroiwa,” alisema Nyika

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic