July 4, 2018


Na George Mganga

Dakika 90 zimemalizika kutoka Uwanja wa Taifa kwa mechi baina ya Simba dhidi ya Singida United kumalizika kwa matokeo ya 1-1 kwenye mchezo wa Kombe la KAGAME.

Walikuwa ni Simba walioanza kujipatia bao la kwanza kupitia kwa straika wake mpya kutoka Gor Mahia FC, Meddie Kagere aliyefunga kwa kichwa kufuatia krosi safi ya Jamal Mwambeleko.

Baada ya Simba kupata bao hilo, Singida waliamka na kuja kwa kasi zaidi wakiutawala mchezo kuwazidi wapinzani wao na katika dakika ya 35, Dan Lyanga aliisawazishia Singida kwa tik-tak.

Mpaka Mwamuzi anapuliza filimbi kuashiria dakika 45 za kwanza kumalizika, Simba walikuwa na bao 1 na Singida wakiwa na 1.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kushambuliana kwa zamu zikijitahidi kusaka bao la nyongeza kwa kila upande lakini jitihada hizo hazikuweza kuzaa matunda.

Mpaka dakika 90 kwa ujumla zinamalizika, Simba 1, Singida United.

Matokeo haya yanaifanya Singida United kushindwa kulipiza kisasi dhidi ya Simba kutokana na sare hiyo, ikumbukwe Simba imeifunga Singida katika michezo miwili waliyokutana tangu ipande ligi kuu bara msimu wa 2017/18.


1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic