July 31, 2018


Baada kuweka kambi kwa takribani wiki moja na siku kadhaa sasa, kikosi cha Simba kesho kinashuka dimbani huko Instanbul kucheza mechi ya kwanza ya kujipima nguvu.

Simba watacheza na Moulodia Club of Oujda ya Morocco ambayo pia imeweka kambi nchini humo kwa maandalizi ya ligi msimu ujao.

Kuelekea mechi hiyo ya kirafiki, timu hiyo kutoka Morocco itawapa nafasi Simba ya kuweza kukipima vema kikosi chao ambacho hakijacheza mchezo wowote tangu kiwasili Instanbul kwa maandalizi ya msimu mpya.

Mechi hiyo ambayo itapigwa majira ya saa 12 jioni, itakuwa ni jaribio zuri kwa Kocha Mbelgiji, Patrick Aussems ambaye amechukua nafasi hiyo kutoka kwa Mfaransa, Pierre Lechantre baada ya mkataba wake kumalizika.

Kupitia mechi hiyo, Aussems atapata nafasi ya kuwatazam vema vijana wake baada ya kukipangua kikosi upya tayari kuanza mchakato wa kuanza kukipanga tena kabla ya pazia la ligi kufunguliwa Agosti 22.

4 COMMENTS:

  1. Huwa najiuliza Media iliyosema Simba amecheza mechi na kufungwa goli 6 bila, huku tunazo habari hizi sasa kuwa kesho ndio itakuwa mechi yake ya kwanza Simba kucheza na timu ya Morocco huko Uturuki, hivi Media hiyo itaheshimikaje kwa kusema uongo? Where is their integrity? Aibu kubwa tu. Unajua hata ukiomba radhi baadae, ni ukweli kwamba habari za kwanza za uongo zimeshaenea na huwezi kote ukafikia ili usahihishe. Suala yule source wa uongo wote achukuliwe hatua na ajulikane kuwa huyu ndiye mtoa habari. Lazima tukomeshe porojo za mtangazaji binafsi kutumia chombo cha habari kuudanganya umma.

    ReplyDelete
  2. Mbona husemi saa 12 jioni ya lini?

    ReplyDelete
  3. Tatizo la kusoma bila kuelewa. Aya ya kwanza inajieleza kwamba mechi itachezwa kesho .Mtu anauliza mechi itachezwa lini?
    Clouds wanajulikana kwa umbeya nä uzushi. Ni media iliyopoteza heshima kabisa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic