July 2, 2018


Baadhi ya wanachama wa Yanga wameibuka na kuutaka uongozi wa klabu yao kuacha kuficha usajili unaofanywa na badala yake waweke mambo hadharani.

Wanachama hao wamekuwa wakilalamika kwa muda mrefu kutokana na uongozi wa Yanga mpaka sasa kushindwa kuweka wazi juu ya usajili ambao umefanywa kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Wanachama hao kutoka tawi la Tandale kwa Mtogole, wameuomba uongozi wao kuweka hadharani wachezaji ambao wameshaingia nao kandarasi ili kuweza kuwajuza mashabiki wa Yanga waweze kujua nani na nani amesajiliwa.

Wakati wanachama hao wakilalamikia juu ya suala hilo, uongozi huo hivi karibuni ulisema usajili wake hautowekwa hadharani na utakuwa wa kimyakimya mpaka pale mambo yatakapokuwa tayari utawataja.

Wakati vuguvugu za usajili Yanga zikiendelea, kikosi cha timu hiyo kipo mawindoni hivi sasa kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia FC utakaopigwa Julai 18 2018.

3 COMMENTS:

  1. UNA USHABIKI WA KIJINGA SANA JAMAA WEWE, MFUATE AKILIMALI AKWAMBIE HAO WALIOSAJILIWA. UNAABUDU NJAA SIO!

    ReplyDelete
  2. YANGA WASIPOANGALIA WANAWEZA WAKAFANYA VIBAYA KWENYE MCHEZO WAO NA GOR MAHIA ZIMEBAKI WIKI MOJA NA NUSU LAKINI BADO ASILIMIA KAMA 70% YA WACHEZAJI WA KIKOSI CHA KWANZA HAWAJAANZA MAZOEZI, WENGI WAO WAKIWA WANADAI MISHAHARA NA MIKATABA MIPYA AMBAYO BADO HAWAJAPEWA HII NI HATARI SANA, MWALIMU AMEANZA MAZOEZI NA KUNDI KUBWA LA WACHEZAJI WAPYA WANAOJARIBIWA, HII NI HATARI SANA, HATA HUYO MANJI KAMA ANA NIA NZURI YA KUISAIDIA YANGA KWANINI ASIRUDI TU KWENYE KAZI NA KUWALIPA MADAI YA WACHEZAJI? HIVI YEYE ATAFURAHI IKIWA TIMU HAITASAFIRI KWENDA KENYA KWAKUWA WACHEZAJI WAMEGOMA?? KWELI KAMA NIA YAKE NI NZURI KWANINI AISIINGILIE KATIKA WAKATI HUU AMBAPO MUDA UNAZIDI KWISHA, NA HAO WACHEZAJI HATA MAZOEZINI HAWAENDI??? HIVI HIYO KAMATI KWANINI HAIFANYI YALE WALIYOAMBIWA WAYAFANYE KATIKA MKUTANO MKUU? MUDA UNAISHA NA HAKUNA LINALOENDELEA NI VURUGU TUPU? HIVI KOCHA KWANINI ANAWAKATAA WACHEZAJI WANAOJARIBIWA? NA KWANINI HATA WANACHAMA HAWAUSHINIKIZI UONGOZI WAFANYE JUU CHINI WACHEZAJI WAANZE MAZOEZI HARAKA KWANI MUDA UNAISHA????

    ReplyDelete
    Replies
    1. ACHA UFALA WEWE NA TAARIFA ZAKO ZA KUOKOTEZA, UNALETA USHABIKI MAVI SIO!

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic