August 6, 2018


Na George Mganga

Baada ya kambi ya wiki mbili kumalizika huko Instanbul katika Milima ya Kartepe, Uturuki, kikosi cha Simba kinaratajia kuwasili leo Dar es Salaam.

Simba walienda kuweka kambi maalum nchini huko kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara pamoja na tamasha la Simba Day.

Wakati Simba wakiwa kambini walicheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Mouolodia FC ambayo walienda naye sare ya bao 1-1 huku mechi ikimalizika sakika ya 65 kutokana na mvua kubwa kunyesha uwanjani.

Vilevile Simba juzi wlaikipiga na Ksaifa ya Palestina na kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 ambayo yaliwekwa kimiani na Emmanuel Okwi aliyefunga mawili pamoja na straika hatari, Meddie Kagere ambaye alisainiwa kutoka Gor Mahia FC ya Kenya.

Katika tamasha la Simba Day ambalo hufanyika kila mwaka ifikapo Agosti 8, Simba watashuka dimbani siku hiyo kukipiga na Asante Kotoko ya Ghana ambayo imeshika nafasi ya 4 ikiwa na tofauti ya alama 3 na Ashanti Gold iliyo nafasi ya kwanza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic