August 6, 2018


Benchi la ufundi la Yanga, chini ya Kocha Mwinyi Zahera limempa mamlaka beki Kelvin Yondani kuwa mchezaji kiongozi ndani ya kikosi hicho akisaidiwa na Juma Abdul ambaye ni swahiba yake mkubwa na ambaye hata kwenye usajili walitikisa.

Yondani ambaye alifanya vizuri na Yanga msimu uliopita anapewa nafasi aliyokuwa akiikaimu msimu uliopita baada ya Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kupoteza namba yake kwenye kikosi cha kwanza.

Siyo hilo tu, Zahera amebainisha kwamba siku si nyingi atatua Kocha Mzanzibari kwenye kambi yao iliyopo Morogoro ambaye jukumu lake itakuwa kunoa makipa wa Yanga na Noel Mwandila atafanya kazi ya kuwaweka fiti kwenye idara ya viungo.

Spoti Xtra linajua kwamba kuna viongozi wa Yanga, wanamtaka Kocha Mecky Maxime wa Kagera kuwa msaidizi wa Zahera lakini Mkongomani huyo mwenye uraia wa Ufaransa anasema hajasikia lolote na yeye ndiye mwenye mamlaka ya kuchagua nani wa kufanya nae kazi.

Kikosi cha Yanga kwa sasa kipo mkoani Morogoro kikiendelea na maandalizi yake ya msimu mpya pamoja na kukamilisha ratiba ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Zahera ambaye anazungumza Kiswahili cha lafudhi ya Kikongo anasema ; “Nimefanya uchaguzi wa nahodha wa timu juzi Ijumaa na Kelvin Yondani alipewa hiyo nafasi, atasaidiana na mwenzake Juma Abdul kuhakikisha mambo yote yanakwenda sawa.”

“Kwa hiyo hawa watafanya kazi na wenzao kuhahikisha mambo yanakwenda sawa hasa suala la nidhamu linakuwa vizuri ndani ya kikosi chetu ambacho kwa sasa tunapambana kuhakikisha timu inakuwa sawa,” anasema Zahera ambaye ni Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa ya DR Congo.

Kocha huyo anasema amefanya uteuzi wa wachezaji hao kwa kuzingatia uzoefu wao, uwezo wao ndani na nje ya uwanja, ushawishi wao kwa wenzao pamoja na ukongwe ndani ya timu na anaamini kwamba wataiongoza vyema Yanga ndani haswa ndani ya Uwanja.

Miongoni mwa majukumu ya Yondani sasa kama nahodha ni kujenga umoja ndani ya wachezaji wa Yanga, kufanya kazi kwa mfano ndani na nje ya uwanja, kujadili na kocha kuhusiana na mambo muhimu pamoja na kutoa maoni kwenye upangaji wa kikosi.

Mbali na hilo pia Yondani anatakiwa kujiamini zaidi ya wachezaji wenzake, kufanya maamuzi kwa akili ndani ya uwanja, kujua ubora na udhaifu wa kila mchezaji ndani na nje ya uwanja pamoja na kuwajengea morali ya kupambana katika mazingira yote.

Yondani pia anapaswa kuwasiliana kwa nguvu ndani ya uwanja kwa chochote kile kinachotokea na pia kujua kinachoendelea ndani ya timu na kuzungumza na wenzie na hatakiwi kuwa mtu wa kupaniki.

CHANZO: SPOTI XTRA

2 COMMENTS:

  1. Domo jumba ya maneno, kasema Mhindi. Yondani mmoja atafanya nini na mpaka sasa inaonesha inaogopa kutafuta timu yenye kiwango cha kujulikana minajili ya kujipima kutokana na hofu ya kufungwa

    ReplyDelete
  2. Domo jumba la maneno kweli mechi wanacheza za kimataifa zinafaa kocha kujua udhaifu Wa timu yake yanga haitaji mechi ngumu kama unavyofikilia WW timu inahitaji morali umoja na utulivu na wachezaji kupata stahiki zao wachezaji wasipo hudumiwa vizuri hata ukiwapa mechi na Madrid hakuna performance nzuri watakayo kupa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic