August 15, 2018


Kufutia sakata linayoendelea kati ya Mwanamuziki Rich Mavoko na Lebo ya WCB inayoongozwa na Diamond Platnumz, suala hilo limetua mikononi mwa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) na kupokea malalamiko ya Mavoko kuhusiana na mkataba wake na lebo hiyo ambao alidai ni wa kinyonyaji.

Baada ya kupokea malalamiko hayo, Basata imemuita Diamond na viongozi wake ambao ni Mkubwa Fella, Sallam na Babu Tale, leo Agosti 14, 2018 na kuzungumza nao katika ofisi za Basata zilizopo jijini Dar es Salaam.

Uamuzi uliotolewa na walezi hao wa sanaa nchini ni kuandaa kikao kitakachokutanisha pande zote mbili yaani Diamond na Mavoko kisha wayazungumze na kufikia muafaka.

2 COMMENTS:

  1. Dalili za kudhalilika kwa baraza zinaanza kujitokeza. Hivi mpaka mtu kupeleka mashtaka kwenye baraza inamaanisha nini? Si kwamba wameshindwana huko walikotoka? Je wakishindwana kupata suluhisho mbele ya baraza nini kitatokea?

    ReplyDelete
  2. Kichwa cha habari tofauti na maudhui!!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic